ZIMAMOTO NA UOKOAJI KATAVI WAELEZA MIKAKATI KUPAMBANA NA MAJANGA YA MOTO


Na.Issack Gerald-Katavi
JESHI la zimamoto Mkoa wa Katavi limedhamilia kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na kujiahadhari na majanga ya moto.

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi msaidizi wa zimamoto mkoa wa Katavi Bw.Edward Kakwale wakati mikakati ya jeshi hilo katika kupambana na majanga ya moto Mkoani Katavi.
Kakwale amezitaja baadhi ya changamoto zinazokwamisha ufanisi wa jeshi hilo kuwa ni elimu ndogo kwa jamii kuhusu namna ya kuzima moto, pamoja na miundo mbinu mibovu ya bara bara hali inayo pelekea kutofika mapema eneo la tukio.
Aidha ametoa wito kwa taasisi za kiserikali na zisizokuwa za serikali, pamoja na migodi kuchukua taahadhari kujikinga na madhara ya moto.
Jeshi la zimamoto lilianzishwa rasimi 2007 ambapo liliingizwa moja kwa moja katika wizara ya mambo ya ndani na kurithi kazi za Kikosi cha zimamoto kilichokuwa chini ya halmashauri za miji.
Mapema mwezi Aprili,jeshi la polisi Mkoani Katavi lililaumiwa kwa kuchelewa kutoa huduma ya kuzima moto wakati bweni la wavulana la shule ya Sekondari Sanny lilipokuwa likiungua ambapo moja ya changamoto waliyoibainisha ni kutokuwa na maji ya kutosha yaliyosababishwa na uhaba wa magari na maji kuwa umbali mrefu kutoka tukio la moto.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA