WAFANYABIASHARA MPANDA WAPEWA SIKU 21 KUHAMA MAENEO YASIYO RASMI KIBIASHARA



MKUU wa wilaya ya Mpanda Mh Paza Mwalima ametoa siku 21 kwa wafanyabishara wote wanaofanya shughuli za kiabiashara katika maeneo yasiyo rasimi kuondoka malamoja.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Afisa tarafa wa kata ya Kashaulili wakati wa ufumbuzi wa mgogoro wa wafanya biashara waliopo eneo la Nsemulwa katika kata ya Uwaja wa Ndege amesema nilazima wafanya biashara wafuate taratibu zote za uaanzishaji wa masoko.
Kwa upande wao wafanyabiashara wamedai kusikitishwa na maamuzi hayo kwani muda uliotolewa ni mfupi nab ado hakuna tamko rasimi kuhusu wapi wanapaswa kuhamia.
Ni wiki ya pili tangu wafanya biashara wadogo wadogo waandamane mpaka ofisi za mkuu wa wilaya kwa madai ya kuwepo kwa ubabaishaji katika zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wote walio katika eneo lisilo lasimi maalufu kama kwa mkumbo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA