MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MTEGONI,APEWA SIKU SABA KUCHUNGUZA MHANDISI MWENYE DHARAU NA JEURI KWA VIONGOZJI WA SERIKALINI NA UBINAFISI WA MATUMIZI YA GARI,UHAKIKI WATUMISHI HEWA NALO LAENDELEA KUMTESA MKURUGENZI



Na.Issack Gerald-Nsimbo
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.michael zyungu amepewa siku 7 kuchunguza kazi ya mhandisi aliyetajwa kwa jina mojala Mh. Mbotu anayetuhumiwa kudharau na kuonesha jeuri kwa viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na ubinafsi katika kutumia mali za Halmashauri likiwemo gari la halmashauri hiyo.

Agizo hilo limetolewa Aprili 15,2016 na mwenyekiti wa halmashauri  ya Wilaya ya Nsimbo  Mh.Raphael Kalinga katika kikao cha madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Aidha ameongeza kuwa katika Halmshauri hiyo kuna watumishi hewa katika idara ya  elimu ya msingi na sekondari ambao wanaendelea kulipwa mishara ambapo pia Mh.Kalinga ameuagiza uongozi wa Halmashauri kupata takwimu ya watumishi hao wanaoendelea kulipwa mishahara ndani ya hizo siku 7 ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Katika hatua nyingine,watendaji wa serikali wametakiwa kutoa ushirikiano  kwa  madiwani ili kutatua changamoto za wananchi huku akisema kuwa watendaji wasiowajibika ipasavyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao
Halikadhalika Kalinga ametoa wito kwa viongozi wa umma kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kusimamia mapato ya ndani ya halmashauri husika ikizingatiwa kuwa Wiki iliyopita  serikali ilitangaza kuzifuta halmashauri zote zitakazo shindwa kukusanya mapato ya ndani kwa kiwango cha 80% .
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya mlele Kanali Mstaafu Issa Sulemani Njiku amewataka viongozi wa Halmshauri kuhakikisha wanasimamia ipasavyo zoezi la kuwatambua watumishi hewa katika maeneo mbalimbali wakiwemo waliopo katika idara ya afya,elimu pamoja na kilimo
Endelea kufuatilia P5 TANZANIA MEDIA,Kwa maoni au ushauri p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA