MGANGA MKUU HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA AKANUSHA WAGONJWA NA WAJAWAZITO KULAZIMISHWA KUPIMWA VVU BILA HIARI.

Na.Issack Gerald-Mpanda
HOSPITALI YA WILAYA Mganga mkuu Hospitali ya Wilaya ya MpandaDk.Naibu Mkongwa,amekanusha taarifazilizosambaa kuwa wanawalazimisha wagonjwa kupima Virusi vya Ukimwi wanapokuwa wamefika hospitalini hapo kutibiwa.

Dk.Naibu Mkongwa amekanusha hali hiyo wakati akijibu hoja za balaza la madiwani kupitia kikao chake cha tatu ambacho kimefanyika jana Mjini Mpanda.
Amesema wanapimwa bila hiari na kwa amri ya mahakama ni pamoja pamoja na watuhumiwa wa ubakaji na mwathririwa wa ubakaji pia wanawekewa viungo bandia vikiwemo figo moyo.
Kwa upande mwingine,Kituo cha Afya cha Mwese ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyopo katika Halmashauri hiyo ambapo kituo kicho kinakabiliwa na tatizo la kutokuwa na maji,uchakavu wa mashuka na ukosefu wa dawa ambapo kwa mjibu wa diwani wa Kata ya Mwese,kituo hicho kimekuwa kikipata chupa moja ya vidonge(Tembe).
Kwa mjibu wa wakuu wa idara ya Afya wa Halmshauri wakijibu hoja za balaza la madiwani,wamesema kuwa milioni 720 zimetengwa kwa ajili ya kunusuru hali ya kituo hicho cha afya.
Wakati huo huo licha ya kuwepo mafanikio ya maendeleo katika baadhi ya kata mbalimbal zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda,kata hizo zimeonekana kuwa na changamoto katika sekta ya afya,miundombinu ya barabara na elimu.
Kwa upande wa Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  Hamad Mapengo na Mkurugenzi mtendaji Estomihn Chang’a wamewashauri  madiwani kuwashirikisha wananchi katika vijiji na kata zao katika utatuzi wa baadhi ya changamoto za maendeleo zilizo ndani ya uwezo wao

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA