KUPATIKANA KWA SHIVYAWATA KATAVI MKOMBOZI KWA WENYE ULEMAVU



Na.Issack Gerald-Katavi
Kupatikana kwa uongozi wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania SHIVYAWATA mkoani Katavi, kutaongeza nguvu katika kutetea haki na kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu Mkoani hapa.

Maslahi au haki ya watu wenye ulemavu kwa muda mrefu hapa Tanzania,yamekuwa yakitetewa na vyama vya watu wenye ulemavu,wadau wa haki za binadamu wakati mwingine SHIVYAWATA linalojumuisha umoja wa vyama hivyo .
Mwenyekiti wa Shivyawata Mkoani Katavi Bw.Issack Mlela amesema kuwa,kabla ya kuunda shirikisho hilo,ilikuwa vigumu kutetea haki za mlemavu kwani kila chama kilikuwa na utetezi wake binafsi na hivyo kutokuwa na hoja ya nguvu ya pamoja.
Aidha mwenyekiti huyu amesema kuwa kupatikana kwa uongozi wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania SHIVYAWATA mkoani Katavi, kutaongeza nguvu katika kutetea haki na kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu Mkoani hapa.
Aidha Bw.Mlela amewaomba watu wenye uwezo wa kipato kusaidia shirikisho hilo kuanzisha miradi ya maendeleo ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo kukosa Ofisi yao maalumu.
Uchaguzi wa viongozi wa shivyawata Mkoani Katavi,ulifanyika mwezi Machi mwaka huu ukishirikisha vyama vitatu vilivyopo Katavi kati ya vitano vilivyopo Tanzania vikiwemo TLB Chama cha wasioona Tanzania na TAAS Chama cha wenye ualbino.
Pamoja na kubainisha changamoto zinazowakabili pia Mlela anatoa wito kwa jamii yenye uwepo wa kipato.
Jumla ya viongozi sita ndiyo wanaongoza Shirikisho la vyama vya watu wenye uelamavu SHIVYAWATA Mkoani Katavi ambao ni Bw.Issack Mlela mwenyekiti wa shirikisho hilo anayetoka katika chama cha wasioona TLB,Martha Iddy katibu Kutoka chama cha watu wenye ulemavu wa viungo CHAWATA,Prasido Kameme kutoka Chawata,Francisco Mazwazwa kutoka chama cha wasioona,Ashura Shabaani kutoka Chama cha wenye ualbino ,Rehema Maganga kutoka chama cha wenye ualbino TAAS,Chama cha wenye mtindio wa ubongo na chama cha wenye ulemavu wa kutosikia yaani viziwi.
‘’Ulemavu ni hali ya kuwa na hitilafu ya kudumu mwilini au akilini inayomzuia mtu kutekeleza shughuli zilizo kawaida katika maisha ya jamii’’ ambao haki zao husimamiwa na sheria namba.9 ya mwaka 2010 ili waheshimike,wathaminiwe,walindwe na wapatiwe haki zao za msingi ikiwemo elimu ,kupatiwa matibabu.
Taasisi ya Foundation For Civil Society limekuwa likonekana kutoa semina mbalimbali kwa vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi ukiwemo Mkoa wa Katavi semina hizo zikilenga kutambua haki za mwenye ulemavu,majukumu ya wenye ulemavu,jamii na viongozi wa kiserikali.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA