JERA MWAKA MMOJA WILAYANI MPANDA KWA KUENDESHA UVUVI NDANI YA HIFADHI



Na.Vumilia Abel-Mpanda
MAHAKAMA ya Wilaya Mjini Mpanda imemuhukumu mtu mmoja mkazi wa  Kakese kwenda jela mwaka mmoja  kwa makosa mawili likiwemo la kujishughulisha na uvuvu ndani ya hifadhi bila kibali.

Akitoa hukumu hiyo,hakimu mkazi Orida Amworo amesema mnamo tarehe 31 mwezi agost 2015 majira ya saa 7 mchana mshitakiwa  Donald Nkwibi aliingia ndani ya hifadhi bila kibali pamoja na kufanya shughuli za uvuvi  mto Kantyentye .
Amworo ameongeza kusema  kuwa kosa la kwanza kuingia ndani yahifadhi bila kibali mshitakiwa atatumikia kifungo cha miezi sita jela na kosa la pili kuvua samaki kilo 30 aina ya kambale atatumikia kifungo miezi sita.
Kwa upande wake mshitakiwa amekili kosa na mahakama imemuhukumu kwenda jela.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA