WANNE WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO KATAVI


Na.Issack Gerald-Mlele
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za kukutwa na vipande vitatu vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 11 vyenye thamani ya shilingi milioni 32,530,650/=ambayo ni sawa na tembo 01 aliyeuawa.

Kamanda msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Frank Koroneli (25) Adela Alex (23) Moris ezron (34) na Sedekia Shadrack(38) ambao ni wote wakazi wa kijiji cha Nduwi kata ya Katumba Wilayani Mlele.
ACP Mohamed amesema kuwa,mnamo tarehe 05.03.2016 maeneo ya Msasani Kijiji cha Nduwi Station Kata ya Katumba,Jeshi la Polisi likiwakatika katika ya doria walipata taarifa toka kwa raia wema kuwa huko katika Kijiji cha Nduwi kuna wakazi wanajihusisha na shughuli haramu za ujangili ambapo baada ya taarifa hiyo kupokelewa ndipo walipofuatilia na kuweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na vielelezo hivyo huku wakiwa wamevificha vipande hivyo kwenye kichaka.
Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili mara baada ya upelelezi kukamilika.
Hata hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ametoa wito kwa wananchi kutojihusisha na shughuli haramu za ujangiri na biashara za nyara za serikali kwani  ni uhalibifu wa rasilimali za taifa letu hasa kwa manufaa ya vizazi vijavyo na amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wote wasiotii sheria pasipo kushurutishwa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA