UJUMBE WA VIONGOZI WA KITAIFA MRADI WA ELIMU JUMUISHI WAWASILI KATAVI KWA ZIARA,WAZUNGUMZA NA KAMATI YA KULEA BALAZA LA WATOTO CHANGAMOTO ZAIBULIWA


NA.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Kamati ya kulea balaza la watoto wanaoishi katika mazingira magumu yenye mradi ujulikano kama mradi wa elimu Jumuishi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamekutana leo na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu.

Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Shirika la IAS Tanzania Bi.Elizabert Mavoa ambaye ametembelea kamati hiyo,amesema lengo la ziara ni kupata taarifa mbalimbali ili kufahamu changamoto zinazowakabili watoto wenye mahitaji maalumu katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa elimu Jumuishi  Tanzania Bi.Irene Shayo ameiasa kamati kushirikisha jamii na serikali kutatua changamoto za watoto wenye ulemavu.
Naye mratibu wa mradi wa elimu jumuishi katika mikoa ya Rukwa na Katavi Bw. Joseph Ndomba amesema kuwa katika Mkoa wa Rukwa na Katavi tangu kuanzishwa kwa mradi katika mikoa hii mwaka 2012,kuna mafanikio makubwa ikiwemo idadai ya wanafunzi wenye ulemavu kuongezeka shuleni ili kupata elimu kama  watoto wengine wasio walemavu.
Wakati huo huo,katika kuhakikisha kuwa wanatatu changamoto ya vitendea kazi,mradi wa elimu jumuishi umepatiwa zana mbalimbali ikiwemo gari na vifaa vingine ambapo mradi huu hufanya kazi katika Wilaya za Mpanda,Nkasi na Sumbawanga.
Mradi wa elimu Jumuishi wa awamu ya pili ulianza mwaka 2015 mbapo kila mradi hudumu kwa kipindi cha miaka 3 kabla ya kusaini mkataba wa mradi mwingine.
Mpaka sasa tangu mwaka 2012,mikoa pekee ya Katavi na Rukwa ndiyo mikoa iliyopewa kipaumbele kwa mradi wa elimu jumuishi.
Mwaka jana 2015,jumla ya wtoto 62 wenye mahitaji maalumu Wilayani Mpanda waliokuwa hawapewi kipaumbele, waliibuliwa na kupelekwa shuleni kusoma.
 Kamati ya balaza la mradi wa elimu jumuishi Wilayani Mpanda,inafanya kazi chini ya ufadhili wa mashirika matatu yaliyoungana na kuunda umoja wao unaojulikana kama IFI.
Mashirika haya  ni International Aids Services(IAS),Free Pentekoste Church Of Tanzania(FPCT) na International Center Of Disabilities
                                                                 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA