MBARONI KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO KATAVI


Na.Issack Gerald-Mlele
Jeshi la Polisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi linamshikilia Bw. Robert Nyakie(40) mkazi wa kijiji na Kata ya kanoge barabara ya tatu kwa tuhuma ya kukutwa na meno ya tembo kinyume na sheria.
                                       
ACP Rashid Mohamed,Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi (PICHA NA.Issack Gerald)
                                             
Vipande vya meno ya tembo vikiwa Mezani(PICHA NA.Issack Gerald)



Mtuhumiwa Bw.Robert Nyakie akiwa chini ya ulinzi (PICHA NA.Issack Gerald Machi 04)

Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed amesema,mtuhumiwa ametenda kosa hilo mnamo Machi mosi mwaka huu katika kijiji cha kanoge barabara ya kwanza.
Aidha,ACP Mohamed amesema,Bw.Nyakie akiwa na vipande  vinne vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 11.50 ambavyo thamani yake ni Shilingi milioni Ishirini na saba na laki saba na Elfu hamsini amabvyo ni sawa na tembo mmoja aliyeuawa.
Mtuhumiwa huyo aliyekuwa amevichimbia vipande hivyo nje karibu na ukuta wa nyumba yake,anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili mara baada ya upelelezi kukamilika.
Hata hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wananchi kutojihusisha na shughuli haramu za ujangiri na biashara za nyara za serikali kwani  ni uhalibifu wa rasilimali za taifa letu hasa kwa manufaa ya vizazi vijavyo na pia  amesisitiza hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wote wasiotii sheria pasipo kushurutishwa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA