BWENI SHULE YA SEKONDARI YA KANISA KKKT MPANDA LATEKETEA KWA MOTO,WANAFUNZI 31 WANUSURIKA

Na.Issack Gerald-Mpanda
Bweni la wavulana la Shule ya Sekondari ya Sanny inayomilikiwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeteketekea kwa moto na kuteketeza mali zote za wanafunzi.

Mkuu wa Shule ya Sanny Sisiter Anna Usiri amesema kuwa tukio hilo ambalo limetokea leo majira ya saa 12 Alfajiri hakuna mwanafunzi aliyepatwa madhara  kiafya mbali na mali zao zote kuteketea.
Aidha,Mkuu huyo wa shule,ametoa hofu wazazi wa wanafunzi hao kuwa hawatakosa  mahali pa kulala licha ya bweni lao kuungua ambapo pia wataendelea na masomo kama kawaida.
Amesema kuwa katika bweni hilo,vitu ambavyo vimetketea ni magodoro,sare za shule,baadhi ya daftari na vitabu.
Kwa upande wake kiongozi wa bweni hilo ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo Bw. Ansel Felisian amesema kuwa waliamka alfajiri ya saa 12 na kwenda darasani kusoma ambapo tukio hilo lilijulikana baada ya mwanafunzi wa kidato cha kwanza kutoa taarifa kwa kiranja huyo baada ya mlinzi wa shule kumwagiza akatoe taarifa juu ya hali hiyo.
Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi  Mrakibu Nestory Kisenya Konongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema wamesaidia kuzima moto huo baada ya kupata taarifa za tukio hilo.
Shule hiyo ina wanafunzi 31 waliokuwa wakiishi katika bweni hilo huku shule hiyo change yenye kidato cha kwanza hadi cha tatu ikiwa na jumla ya wanafunzi 66 pekee.
Hata hivyo chanzo cha ajali hiyo ya moto hakijafahamika na uchunguzi unaendelea kufanyika

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA