VIONGOZI MKOANI GEITA WATAKIWA KUTOWAONEA AIBU WAFANYABIASHARA WASIOFUATA KANUNI ZA USAFI ILI KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU


Na.Issack Gerald-Geita
Viongozi wa Mkoa wa Geita wametakiwa wasiwaonee aibu kuwafungia wafanyabiashara wasiofuata kanuni za usafi wa mazingira na hivyo kupelekea mlipuko wa kipindupindu.

Hayo yamesema na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kambi ya wagonjwa ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha afya Nyankumbuli mjini Geita.
Waziri Ummy alisema mlipuko wa  kipindupindu upo hivyo kuwafumbia macho wale ambao wanafanya biashara katika mazingira yasiyo safi na salama lazima watu hao wafungiwe
“ Wanasiasa wenzangu inabidi mtuelewe ,hivi  sasa kuna mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika mikoa ishirini na moja na ni haki ya kuhakikisha afya za wananchi zipo safi na salama hivyo tutaruhusu biashara zilizopo kwenye mazingira safi na salama na endapo tutakua tumejiridhisha kwamba  wafanyabiashara wamezingatia kanuni za usafi wa mazingira”
 Aidha, ameupongeza mkoa wa Geita kwa jitihada za kudhibiti wagonjwa wapya kwa wiki hii kuliko wiki iliyopita ambapo kwa wiki hii kuna wagonjwa wapya wanne,ukilinganisha na wagonjwa nane wa wiki iliyopita,hivyo  ameutaka mkoa kuendelea kutoe elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa huu.
Wakati huohuo waziri Ummy amewataka watumishi wote wa kada za afya nchini kufanya kazi kwa mujibu wa maadili na kwa kuzingatia viapo vya fani zao wakati wanapotoa huduma kwa wananchi
Ummy alisema serikali haitowaonea aibu  kuwachukulia hatua kali kwa kila mtumishi atakayetoa lugha mbaya na kukiuka maadili ya kazi zao wakati wa kutoa huduma kwa wananchi.
“Hatua kali tutachukua kwa yule atakayebainika ametoa lugha isiyostahiki na inayomdhalilisha  mgonjwa, hatutomvumilia kwakweli na hili tutashirikiana na wenzetu wa Tamisemi kulifanyia kazi.
Awali, akisoma taarifa ya Mkoa wa Geita kuhusu hali ya kipindupindu ,Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Joseph Kilasa alisema Mgonjwa wa kwanza alipatikana mwezi wa tisa mwaka jana ambapo  walipata mgonjwa wa kwanza toka mji wa katoro ambaye alitokea jijini dare es salaam.Hadi sasa wamepata jumla ya wagonjwa 116 na watu saba  7 walipoteza maisha

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA