KAMANDA WA POLISI RUKWA AZUNGUMZIA HALI YA USALAMA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA,ASEMA MATUKIO MAKUU MAWILI YALITIKISA MWAKA 2015


Na.Issack Gerald-SUMBAWANGA
Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa limesema kuwa,hakuna matukio matukio ya uharifu yaliyotokea katika kipindi chote cha msimu wa sikukuu za kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016.
                                                        
Ramani inayoonesha mahali Mkoa wa Rukwa unapopatikana pia maeneo yanayopakana na mkoa huo yanaonekana

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani  Rukwa SACP Jacob Mwaruanda wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Kwa nji aya simu,kuhusu Tathmini ya hali ya usalama katika sikukuu za krismas Desemba 25 na mwaka mpya 2016.
Amesema kuwa tukio pekee lililotokea msimu wa sikukuu ni linamhusisha mtu mmoja mtembea kwa mguu aliyekufa baada ya kugongwa na pikipiki Mjini Sumbawanga.
Aidha Kamanda Mwaruanda amesema,matukio makubwa yalitokea kwa mwaka 2015 ni pamoja na Mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Albino na kuchomwa vifaa vya kupigia kura pamoja na gari wakati wa uchaguzi wa mwaka jana wa urais,ubunge na udiwani.
Katika matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino Mkoani Rukwa,ni pamoja na tukio la mwezi machi mwaka 2015 ambapo Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino Baraka Cosmas (6) aliyekuwa akiishi na wazazi wake kijijini Kipeta, Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa kiganja cha mkono wake wa kulia na watu wasiojulikana kisha kutokomea nacho kusikojulikana.
Hata hivyo Kamanda Mwaruanda amesema mashauri ya watuhumiwa wa ukatiri kwa mtoto huyu mwenye albino yanaendelea mahakamani.
Wakati huo huo wakazi wa Mkoa wa Rukwa,wametakiwa kushirikiana na Polisi kwa kuripoti matukio ya uharifu kabla hayajasababisha madhara kwa watu.
Asante kwa kuendelea kuwa namii,endelea kuhabarika na P5 TANZANIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA