ACHOMWA KISU WILAYANI MPANDA UTUMBO WATOKA NJE,MHUSIKA ATOKOMEA KUSIKOJULIKANA POLISI KUMSAKA MHUSIKA.


Na.Issack Gerald-Katavi
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Elia Edward(40), makazi wa mchangani alichomwa tumboni na kitu chenye ncha kali na kisha utumbo wake kutoka nje na mtu asiyemfahamu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 24.01.2016 majira ya saa 19:00 jioni katika eneo la Mzabwela Kijiji cha Mchangani Kata ya Ikola Tarafa ya Karema Wilayani  Mpanda Mkoani Katavi.
Taarifa ya Kamanda kidavashari inataarifu kuwa mara baada ya mtuhumiwa kutenda kosa la kumchoma kisu majeruhi alikimbilia kusikojulikana.
Amesema ,majeruhi amepelekwa katika hospitali ya Wilaya Mpanda kwa matibabu zaidi huku Chanzo cha tukio hili kikiwa bado hakijajulikana
Hata hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha mchangani linamsaka mtuhumiwa alipokimbilia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi ambapo amesema kuwa sheria kali zitaendelea kuchukuliwa pale wahusika watakapobainika.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA