BREAKING NEWS : WAHAMIAJI HARAMU 8 RAIA WA ETHIOPIA WANASWA IRINGA-P5 TANZANIA INAKUSOGEZEA HIYO


Na.Issack Gerald-Iringa
Jeshi la polisi Mkoani Iringa limewakamata wahamiaji haramu 8 Raia wa Ethiopia waliokiuwa wakisafiri isivyo halali na bila kibali cha kuingia nchini wakiwa wamepakiwa na gari lililokuwa limebeba magazeti.
                                              
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Peter Kakamba

Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Peter Kakamba amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika kituo cha ukaguzi wa magari mvilo Manispaa ya Iringa wakati Polisi likiwa kwenye oparesheni ya kawaida.
Kamanda Kakamba amewataja baadhi ya wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni pamoja na Godfrey Tanka (32) ambaye ni dereva akisaidizana pia na Michael Japhet (37) wote wakazi wa Dar es Salaam.
Wakati huo huo mtu anayedhaniwa kuwa msindikizaji wa gari hilo naye anashikiliwa na Polisi Mkoani Humo ili kubaini kama alikuwa akisindikiza magazeti au watu hao.
Kwa upande wake mmoja wa wasindikizaji amesema kuwa wamepakia watu hao baada ya kusimamishwa na wapiga debe ambapo kwa maelezo ya watu hao wa Ethiopia walisema kuwa wanaelekea Mkoani Mbeya.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA