MAKATIBU WAKUU NA NAIBU KATIBU WAKUU WAAPISHWA,WAZIRI MKUU AWAPONGEZA


Na.Ofisi ya waziri Mkuu.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, mara baada ya kuapishwa Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
                                                   
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea na Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakuu baada ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
                                                     
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,Amon Mpanju akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam

   
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Profesa James Epifani Mdoe akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
                                                  
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju wakishuhudia Katibu Mkuu Kiongozi akiwapa maelekezo Makatibu wakuu na Naibu Katibu namna  ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo
Ametoa pongezi hizo wakati Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakiwa wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi hao, kuwa waaminifu, kuwajibika na  kutoa taarifa ya utendaji kwa wananchi. Aidha, alisema kuwa, viongozi wengine watakao apa mbele ya Kamishna wa Tume ya Maadili ni pamoja na  Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali kudhibiti na kufuatilia matumizi ya rasilimali fedha.
“Wakuu wa Wilaya watahakikisha fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike katika shughuli zilizokusudiwa” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano, kwakuwa itatimiza ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais na Makamu wa Rais walizitoa wakati wa Kampeni.
Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu hao, wameapishwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli, ambapo shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke wa Mheshimiwa Rais mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA