WATAHINIWA 5422 KATI YA 6378 DARASA LA SABA WAFAULU KUJIUNGA NA MASOMO YA SEKONDARI KATAVI 2016


MPANDA-Na.Meshack Ngumba
JUMLA ya Watahiniwa 5,422 Kati ya watahiniwa 6,378 waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi Mkoani Katavi wamefaulu Kujiunga na Kidato cha Kwanza Kwa Mwaka 2016.

Akisoma Matokeo hayo jana Katika Kikao cha bodi ya Uchaguzi  wa Wanafunzi watakao jiunga na Masomo ya Sekondari Afisa elimu Mkoa wa Katavi Bw,Ernest Hinju amesema ufaulu huo ni sawa na asilimia 85.1
Kutokana na Matokeo hayo Mkoa wa Katavi umeongoza na kuwa  nafasi ya Kwanza Kitaifa Katika Mikoa iliyofanya Vizuri Katika Mtihani wa Kuhitimu elimu ya Msingi Kwa Mwaka 2015.
Pamoja na Mkoa wa Katavi kushika nafasi hiyo pia Halmasahauri ya Manispaa ya Mpanda imeendelea Kuongoza Kwa Kuwa nafasi ya Kwanza Kitaifa  kati ya halmashauri zote nchini.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA