KIPINDUPINDU KATA YA KAWAJENSE KAMA CHOO HAITAJENGWA




Na.Agness Mnubi-MPANDA
WAFANYABIASHARA wa soko la Majengo mapya kata ya Kawajense Manispaa ya Mpanda wanakabilwa na ukosefu wa huduma ya choo sokoni hapo, hali inayoweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Wakizungumza na Mpanda radio wafanya biashara hao wamesema tatizo hilo ni la kudumu na  uongozi wa Serikali unataarifa juu ya changamoto hiyo.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Kawajense   John Salanga  amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa zaidi ya miaka mine sasa.
Mtendaji amesema atahakikisha anajenga choo sokoni hapo kwa kushirikina  na wafanyabiashara wa ndani na nje ya soko na  iwapo  utekelezaji  huo utashindikana atafunga soko hilo ili kuepuka  magonjwa ya mlipuko.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA