WANANCHI MKOANI KATAVI WATAKIWA KUCHANGIA DAMU SALAMA


Na.Issack Gerald-MPANDA.
WANANCHI Mkoani Katavi wametakiwa kujitokeza kwa hiari ili kuchangia damu Salama.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA,Mratibu wa damu salama Mkoani katavi  Henery Silvery Munah, amesema uratibu wa damu salama kwa Mkoani Katavi ulikuwa ukiratibiwa Mkoani Rukwa ambapo kuanzia mwezi Octoba mwaka huu wameanzisha zoezi hilo kwa mujibu wa sheria na taratibu za wizara ya afya na ustawi wa jamii.
Amesema kuna umhimu  mkubwa wa uchangiaji  damu kwani zaidi ya chupa  800 za damu salama ambazo hutumika kwa kila mwezi mwezi Mkoani Katavi.
Aidha ameihakikishia jamii kuwa damu hiyo inapotumika kwa mgonjwa  hospitalini haiuzwi bali hutolewa bure, na kusisitiza kutoa taarifa iwapo utauziwa damu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA