BREAKING NEWS : VIONGOZI CHADEMA WILAYANI MPANDA WABWAGA MANYANGA


Na.Issack Gerald-MPANDA.
BAADHI ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wamejiuzuru wadhifa wao kutokana na usaliti  ndani ya chama uliotokea  kipindi cha uchaguzi mkuu wa ubunge urais na madiwani Oktoba 25 mwaka huu.

Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA katika ofisi za chama hicho  baadhi ya viongozi hao wamesema wamejihudhuru kutokana na shinikizo la wananchama wa chama hicho kuwataka wajihudhuru.
Naye mwakilishi wa wanachama Joseph Mpela ambaye pia alikuwa mgombea udiwani kata ya magamba amekabidhi barua kwa katibu wa chama kwa niaba ya wananchi inayowataka viongozi hao kujiuzuru.
Kwa upande wake katibu wa Chadema Mkoa wa Katavi Almas Ntije amekiri kupokea barua kutoka kwa wananchi hao na kuomba muda wa kuisoma ili kujua yaliypo katika barua hiyo.
Hata hivyo orodha ya majina ambao wamejiudhuru yanatarajiwa kuwekwa hadharani muda wowote baada ya Katibu kutoa tamko



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA