WAKAZI LAKI MBILI (200,000) WATESWA NA NJAA JIMBO LA UYUI TABAORA BAADHI HAWANA HATA UWEZO WA KUNUNUA KWA BEI NAFUU


Na.Issack Gerald-Tabora
Watu  zaidi ya 200,000 katika jimbo la Igalula Wilayani Uyui Mkoani
Tabora wanakabiliwa na uhaba wa chakula ambapo zaidi ya wakazi 20,000 wakiwa hawana uwezo wakununua hata chakula cha kwa bei nafuu.
Akizungumza na gazeti hili mbunge wa jimbo la igalula (CCM) Mussa
Rashid Ntimizi alisema jimbo hilo linakabiliwa na uhaba wa chakula kwa wakazi zaidi ya 200,000 ambap o wakazi 188,000 wanauwezo wa kununuachakula kwa bei nafu huku wengine 20,000 wakiwa hawana uwezo. .
Alisema kamati ya maafa imefanya tathimini ya waathirika wote na
kubaini kuwa kunahitajika tani 2508 za chakula ili kuweza kuwasaidia
wahanga hao wa njaa jimboni hapo.
Alisema chanzo cha maafa hayo ni mafuriko ya mvua na vipindi vya jua vilivyo pita wakati wa msimu wa kilimo hali iliyosababisha watu wengi
kutokuwa na chakula cha akiba majumbani mwao.
Aidha aliongeza kuwa baada ya kufanya tathimini hiyo na kubaini chanzo cha maafa hayo tayari wameandika barua kwenda Ofisi wa Waziri Mkuu kitengo cha maafa kupitia kamati ya maafa ya mkoa ili kupata msaada huo kwa haraka.
Ntimizi alisema kwa kuwa kuna wakazi ambao wanauwezo wa kununua
chakula kwa bei nafuu na wasikuwa na uwezo kabisa ni vyema serikali
ikafanya haraka kuwanusu wakazi hao ambao wanakabiliwa na njaa.
Akizungumzia hali hiyo kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya Uyui na
diwani wa kata ya goweko Shabani Katalambula alisema wananchi wa jimbo hilo kwa sasa wanawakati mgumu wa kimaisha kwa kuwa hawana chakulancha kutunza familia zao.
Alisema licha ya Mbunge wa jimbo hilo kutoa msaada wa Tani moja na
nusu ya chakula na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mhandisi  Athumani Mvutakamba kujitolea kiasi cha tani moja ya chakula huku akiwataka wadu wengine kujitokeza wakata wakisubili msaada kutoka serikalini.
Kwa upande wake Sada Mohamed ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha tatu na anayetegemea kuingia kidato cha nne mwakani katika shule
sekondari Tura Jimboni hapo alisema wanawakati mgumu wa kimasomo
kutokana na janga la njaa linalo wakabili kijini hapo.
Alisema ni viigumu kwa mwanafunzi kwenda shuleni kama hajala chakula cha kutosha kwani hata masomo yanahitaji afya njema ili kuweza kufanya vizuri kimasomo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA