WATANZANIA WAISHIO NCHINI THAILANDA WACHAGUA VIONGOZI WAO


 
Watanzania waishio mjini Bangkok nchini Thailand wakipata chakula baada ya kufanya uchaguzi

Na.Mwandishi.BANGKOK
Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand (TIT) imekutana na kujadiliana mambo mbalimbali ya jinsi gani wanaweza kusaidiana katika mambo mbalimbali.

Mkutano mkuu wa Jumuiya ulifanyika Novemba 7 katika Hoteli ya Amari Boulevard Mjini Bangkok na kuhudhuriwa na wanajumiya mbalimbali.
TIT ilianzishwa mnano mwezi Aprili mwaka huu na inahusisha watanzania mbalimbali, wanafunzi,wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya kazi nchini Thailand.
Pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kulifanyika uchaguzi wa viongozi ambapo wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa jumuiya kwa kipindi cha mwaka mmoja:Mwenyekiti: Bwana Maumba Mgaya,Makamu menyekiti Bw. Alois Ngonyani,Katibu: Bw.Andrew Wajama,Katibu Msaidizi: Bw. Emmanuel Mushi,Mhazini: Bw. Adolf Kigombola,Mhazini Msaidizi: Bi.Tumaini Kalindile,Afisa Mawasiliano: Bw. Emmanuel Nyamageni,Afisa Mawasiliano Msaidizi: Bw. Jordan Hossea.
Pamoja na uchaguzi kulifanyika sherehe fupi ya kumpongeza Bi Magreth Dionis Mjindo ambaye amemaliza Shahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii na anarejea nyumbani kulitumikia Taifa.
Mawasilano ya viongozi wa Jumuiya hiyo ya Watanzania waishio nchini Thailand (TIT)
                          +66947230002/+66972494819

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA