WABUNGE WATEULE WA BUNGE LA TANZANIA KUANZA KUSAJILIWA LEO


 
Baadhi ya wabunge la Tanzania wakiangalia mandhali ukumbi  bungeni Mjini Dodoma

Na.Mwandishi wetu-DODOMA
Wabunge wateule wa bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatarajia kujisajili leo tayari kwa vikao muhimu vya kwanza vya Bunge wiki ijayo.

Wakati wabunge hao wakianza kujisajili kuanzia kesho na kesho kutwa, Jumatatu ijayo itakuwa ni siku ya kupeana maelekezo, kutembelea Ukumbi wa Bunge na mikutano ya kamati za vyama vya siasa.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ofisi ya Bunge iliyotolewa wiki iliyopita, Jumanne Novemba 17, itakuwa siku ya kuanza kwa kikao cha kwanza kwa kusomwa Tangazo la Rais la Kuitisha Bunge.
Aidha kikao hicho kitafuatiwa na uchaguzi wa Spika, Kiapo cha Uaminifu na Kiapo cha Spika na kisha Kiapo cha Uaminifu kwa wabunge wote.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA