WAKULIMA WAOMBA PEMBEJEO ZA KILIMO ZILETWE MAPEMA


Na. Lutakilwa Lutobeka-MPANDA
Kucheleweshwa kwa pembejeo kwa wakulima imeelezwa kuwa ni sababu inayozorotesha sekta ya kilimo wilayani Mpanda, mkoani Katavi.

Baadhi ya wakulima wilayani Mpanda wamesema hayo wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Wamesema kuwa serikali imekuwa ikichelewesha pembejeo kama mbolea na mbegu hivyo kushindwa kwenda sambamba na msimu wa kilimo.
Aidha wakulima hao wameiomba serikali kuleta mapema pembejeo ili walime na kupata mazao yanayoridhisha.
Naye Kaimu afisa kilimo wa wilaya ya Mpanda Bw. Kennedy Nveramo amesema wamekwishapata pembejeo kutoka mkoani na muda wowote wataanza kusambaza kwa wakulima.
Katika msimu wa kilimo uliopita baadhi ya wakulima walilalamikia serikali kwa kutoa mbegu za mahindi ambazo hazikuwa na ubora unaotakiwa na nyingine hazikuota.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA