RUKWA WAJIPANGA KUHIFADHI MAZINGIRA


NA.Issack Gerald-SUMBAWANGA
Mkoa wa Rukwa Umepanga kupanda miti milioni Tano na laki tano katika Halmshauri zake kwa mwaka wa 2015/2016 lengo likiwa ni kuhifadhi mazingira.

Hatua hiyo imeelezwa na Mshauri  wa mazingira na maliasili Mkoani  Rukwa Nichoraus Mchome wakati akizungumza na Mpanda Radio Ofisini Kwake.
Aidha Mchome amesema kuwa katika kuhakikisha usafi unadumishwa Mkoani humo hususani Manispaa ya Sumbawanga  na maeneo mengine ya Mkoa wa Rukwa, imeteuliwa  siku ya Alhamisi kuwa siku ya Usafi  Kimkoa.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wanaofanya usafi Manispaa ya Sumbawanga,wamesema wanafanya kazi katika mazingira magumu huku wakitumia gharama zao kununulia vifaa vya kufanyia usafi huku wakisema kuwawanafanya kazi hizo kutokana na kutokuwa na namna nyingine ya kuendesha maisha ya kila siku.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA