WAKAZI MKOANI KATAVI WANAOZUNGUKA HIFADHI WATAKIWA KUTOFANYA SHUGHULI YOYOTE HIFADHINI


Na.Issack Gerald-MPANDA
Wananchi wanaoishi karibu na hifadhi mbalimbali Mkoani Katavi wameshauriwa  kutofanya shughuli yoyote ndani ya hifadhi pamoja na  kuzingatia sheria  ya uhifadhi ili kuendelela kuzilinda hifadhi hizo.

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa hifadhi za misitu Wilayani Mpanda Mpanda Bw. Michael Kimata wakati akizungumza na mpanda radio kuhusu ufafanuzi wa sheria ya uhifadhi pamoja na shughuli zinazokataliwa kufanywa ndani ya hifadhi.
Amesema wananchi wanapaswa kutambua kuwa  jukumu la kulinda hifadhi siyo la wahifadhi pekee bali ni wananchi wote wanaoishi jirani na hifadhi.
Aidha Bw. Kimata amesema wananchi wakishiriki kulinda hifadhi na kuheshimu sheria za uhifadhi kutasaidia kuondoa migogoro mingi ambayo imekuwa ikijitokeza kati ya wahifadhi na wanaovunja sheria hizo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA