MAJALIWA KASSIMU MAJALIWA WAZIRI MKUU WA 11 TANZANIA TANGU UHURU WA TANGANYIKA


 
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika kikao cha kwanza katika mkutano wa kwanza wa bunge la 11 kumchagua Waziri mkuu wa Tanzania na Naibu Spika

Na.Mwandishi wetu-DODOMA
Mbunge wa Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameidhinishwa na Bunge la Tanzania kuwa waziri mkuu mpya wa Tanzania.

Mh. Majaliwa amepata kura 258 kati ya 351 zilizopigwa, baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kutangazia bunge kwamba ndiye aliyekuwa amependekezwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa Waziri Mkuu.
Bw Majaliwa(55) mbali na kuwa amekuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa na Jimbo la Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) tangu 2010 pia alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa.
 Waziri Majaliwa anatarajia kuapishwa kesho katika ikulu ya Dodoma.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA