ZAIDI YA SILAHA 17 ZAKAMATWA,WATUHUMIWA WANNE WAFIKISHWA MAHAKAMANI


Issack Gerald-Katavi
Zaidi ya silaha 17 zimekamatwa na kusalimishwa kwa jeshi la polisi Mkoani Katavi huku watu wanne wakifikishwa Mahakamani kwa kipindi cha mwezi Juni hadi Septemba Mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhairi Kidavashari wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu mafanikio ya agizo la kusalimisha silaha alilolitangza mwezi Juni mwaka huu akiwataka wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha.
Katika hatua nyingine akizungumzia siku ya amani duniani amesema kufuatwa kwa sheria na ushirikiano kati ya Jeshi la polisi na raia kutachangia amani kudumu Mkoani Katavi na Tanzania kwa ujumla.
Wakati huo huo akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inalinda Amani na kuheshimu demokrasia hasusani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu.
Siku ya amani duniani inayoadhimishwa  kimataifa kila ifikapo Septemba 21 ya kila mwaka, kitaifa  imeadhimishwa Mkoani Mwanza wakiti kimataifa maadhimisho yakifanyika Nchini Rwanda.
Kauli mbiu katika maadhimisho ya siku ya amani mwaka huu ni ‘’Ushirikiano wa amani, utu kwa wote”

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA