UHABA WA MAJI ZAIDI YA WAKAZI 750 WAATHIRIKA


Issack Gerald-Katavi
ZAIDI YA WAKAZI 750 waishio mtaa wa Kampuni kata ya Misunkumilo wanakabiliwa na  ukosefu wa  maji safi na salama hali inayosababisha kutumia muda mwingi kutafuta maji kuliko kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
Mapema leo wakazi hao wakiongea na mpanda fm wamesema kero ya ukosefu wa maji ni ya muda mrefu ambapo mpaka sasa wana kisima kimoja ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya wananchi katika eneo hilo.
Aidha baadhi yao wamewatuhumu viongozi na wanasiasa kutumia kero ya maji kama chambo cha kujipatia kura na kusahau ahadi hizo mala tu wanapo shika madaraka.
Kwa upande wa mwenyekiti wa mtaa huo Bw James Solomoni amewataka wananchi wa eneo hilo kuwa na subira wakati serikali ikikabiliana na utatuzi wa changamoto hizo.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA