BUASARA,HEKIMA,LUGHA ZENYE HESHIMA ZATAKIWA KUTUMIKA MIKUTANO YA KAMPENI ZA KISIASA KATAVI


 Na.Issack Gerald-Katavi
Busara,hekima na lugha zenye heshima  zimetakiwa kutumiwa na wanasiasa na jamii kwa ujumla katika kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi ili kuepuka kuitumbukiza nchi katika machafuko yanayohatarisha usalama wa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari katika kikao maalumu na wanasiasa,viongozi wa dini na wazee maarufu ambacho kimefanyika katika makao makuu ya Polisi Mkoani Katavi.
Kwa upande wa washiriki wa kikao hicho wamesema kuwa viashiria vya uvunjifu wa amani Mkoani Katavi katika kipindi cha Kampeni vimeshamiri ambapo wameliomba jeshi la polisi kuthibiti hali hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya siasa.
Wakati huohuo vyama vinavyoonywa kufanya vurugu kutokana na kurushiana maneno ya kejeli ni pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Chama cha Mapinduzi CCM.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa vyama vya saiasa wamelitaka jeshi la polisi kutenda haki kwa kila chama katika kushugulikia malalamiko yanayowasilishwa kwao na kukomesha misemo inayotumiwa na Chama cha Mapinduzi CCM kuwa wao ndiyo chama chenye dola na hakuna wa kuwatisha kauli ambayo inaonekana kuwakwaza baadhi ya wafuasi wa vyama vingine.
Kaikao hicho ni mwendelezo wa kikao kama hicho kilichofanyika Septemba 11 mwaka huu ambapo pia kikao kingine kinatarajiwa kufanyika Oktoba 9 wiki mbili kabla ya uchaguzi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA