WAKAZI NSEMULWA KUWASHTAKI MAAFISA ARDHI MANISPAA YA MPANDA KWA WAZIRI WA ARDHI WAKIPINGA USUMBUFU UPIMAJI WA VIWANJA

NA.Issack Gerald-KATAVI
WAKAZI wa mtaa wa Nsemulwa Kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamekusudia kumuita Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kutatua migogoro ya ardhi, wakiwatuhumu maafisa ardhi Wilayani Mpanda kushindwa kutatua migogoro hiyo kwa miaka mitatu sasa.

Wakizungumza na Mpanda Radio, wakazi hao zaidi ya elfu moja wamesema kuwa wamechoshwa na usumbufu wanaoupata kutoka Ofisi ya Ardhi Wilayani, baada ya kutakiwa kutoa kiwango cha pesa kilicho nje ya uwezo wao tofauti na kiasi walichoambiwa awali.
Aidha wamesema kuwa hawako tayari kuhama kupisha wawekezaji na badala yake Ofisi ya ardhi ibatilishe tangazo la kuwataka wakazi hao kuhama eneo hilo, ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.
Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda, Bw. Suleiman Lukanga ameahidi kufuatilia suala hilo na kutoa majibu leo.
Ofisi za idara ya ardhi Katika Manispaa ya Mpanda siyo mara ya kwanza kutuhumiwa kwa kuchelewesha utatuzi wa migogoro ya ardhi bali malalamiko yamekuwa yakitokea katika maeneo mara kwa mara.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA