UHAKIKI MAJINA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MANISPAA YA MPANDA WAKWAMA,MKURUGENZI KUTOA TAARIFA BAADA YA VIFAA KUAWASILISHWA


NA.Issack Gerald-KATAVI
ZOEZI la uhakiki wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura limeelezwa kuchelewa kuanza katika Manispaa ya Mpanda kutokana na kucheleweshwa kwa vifaa, zikiwemo mashine za BVR.

Akizungumza na Mpanda P5 TANZANIA Ofisini kwake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Bw. Suleiman Lukanga amesema anatarajia kutoa taarifa kwa waliojiandikisha katika daftari la mpiga kura ili wakahakiki majina yao baada ya vifaa vyote kuwasilishwa.
 Aidha amesema kuwa zoezi la sasa siyo kwa ajili ya ambao hawakujiandikisha awali wakati wa kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura,bali ni kwa ajili ya kusahihisha makosa yaliyojitokeza wakati wa zoezi hilo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza kuanza kwa zoezi la uhakiki wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura kwa Mkoa wa katavi Agosti mosi  mwaka huu ambapo hata hivyo wakazi manispaa yam panda walikuwa wameanza kushikwa na wasiwasi kutoana na kutoona majina yao katika vituo walivyojiandikisha.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA