WAKAZI MPANDA WANDELEA KUWA GIZANI UMEME KUKATIKA,VIWANDA VYAKOSA UMEME SHUGHULI ZASIMAMA KWA MWEZI SASA



NA.Issack Gerald
TATIZO la kukatika Umeme mara kwa mara Mkoani Katavi  limesababisha kuzorota kwa biashara ya mchele, kutokana na kukwama kwa ukoboaji wa mpunga zao linalotegemewa na wakazi wengi  mkoani Katavi.
Wafanyabiashara wa Mchele pamoja na wamiliki wa Mashine za Kukoboa mpunga wameiambia P5 TANZANIA kuwa, shughuli za ukoboaji wa Mpunga zimesimama kwa sababu ya ukosefu wa nishati ya umeme na kusababisha kupunguza kipato chao.
Mpaka sasa mwezi mmoja unakadiriwa kupita ikiwa Mkoa wa katavi unakabiliwa na  tatizo la kukatika kwa umeme.
Mchele ambao unakobolewa Mkoani katavi husafilishwa kwenda mikoa mbali mbali  nchini Tanzania pamoja na nchi jirani za Rwanda na Burundi, na kukuza kipato cha wafanyabiashara wa mchele.
Hata hivyo taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na Meneja wa Tanesco Mpanda Bw. Chacha Nsiku zinasema kuwa kukatika kwa umeme kunatokana na matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA