MAJAMBAZI YAPORA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI SABA,YAJERUHI PIA


Na.Issack Gerald-KATAVI
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu wanne Wilayani Mpanda kwa tuhuma za kujeruhi na kupora kiasi cha shilingi milioni saba.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dhahiri Kidavashari,amesema kuwa tukio hilo limetokea jana katika kijiji cha Vikonge kata ya Kabungu.
Kidavashari amewataja waliokamatwa katika msako wa jeshi la polisi kuwa ni Mayunga Saguda Makobo(44) mkazi wa Mnyagala,Halila Tiga Bujoribu(33) na Mnyaga Maziku(30) wakazi wa Luhafe na Shija Mahoma(30) mkazi wa Kawajense.
Amesema kuwa watu hao wanaosakika kuwa majambazi waliokuwa wakitumia silaha mbili za kivita aina ya SMG UA-3379 yenye risasi 13 na SMG namba 19111685 yenye risasi 23   walifanya uporaji huo kwa wafanyabiashara Siasa Simon Kasumuni(24) ameporwa shilingi Milioni Tano,simu moja aina ya Techno na Kadi ya benki ya CRDB wakati huo Edward Mnonga(37) ameporwa zaidi ya zshilingi Milioni mbili,simu moja aina ya Techno,kitambulisho cha kupigiakura ambapo kwa upande wake pia alijeruhiwa kwa kupigwa fimbo mkononi na kumsababishia maumivu makali ambapo wote walikuwa wamelala nyumbani kwa Mnyaga Maziku Mkazi wa Luhafe.
Wakati huohuo Kamanda Kidavashari ametoa wito kwa  wakazi Mkoani Katavi waliopo mbali na vituo vya jeshi la polisi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kubaini uharifu kabla ya haujatokea ili kuudhibiti.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA