RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA KIFO CHA MARIA NA CONSOLATA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameungana na Watanzania kuomboleza msiba wa watoto Maria na Consolata,waliofariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya mkoa wa Iringa.
Rais Magufuli katika ukurasa wake wa Twitter ametuma ujumbe akielezea kusikitishwa kwake na msiba wa watoto hao ambao hivi karibuni aliwatembelea walipokuwa hospitali ya Muhimbili wakipatiwa matibabu hivi karibuni.
Vifo hivyo vimetokea siku chache baada ya kuruhusiwa kutoka Hospotali ya Taifa Muhimbili ambako walikuwapo zaidi ya miezi miwili wakipatiwa matibabu.
Taarifa kutoka Hospitali mkoani Iringa zinaeleza kuwa watoto hao walifariki kwa muda tofauti ambapo mmoja alifariki saa 1 usiku na mwengine alifariki saa 3 usiku.
Maria na Consolata ambao ni pacha walizaliwa hapa nchini wakiwa wameungana na wakaishi hadi kujiunga na chuo kikuu wakiwa bado wameungana.
Pacha hao waliokuwa na umri wa miaka 22 wamekuwa wakitunzwa na watawa wa kanisa Katoliki tangu na baada ya kuzaliwa na mwaka jana walijiunga na chuo kikuu cha Ruaha Catholic University na kuanza na masomo ya kompyuta kabla ya kuanza masomo kamili Oktoba.
Maria na Consolata walikuwa wamefanya mitihani yao ya mwisho ya kidato cha sita,katika shule ya Sekondari ya Udzungwa mjini Iringa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA