BASI LAUA LAJERUHI MKOANI RUKWA


MTOTO mwenye umri wa miaka minne amefariki dunia papo hapo baada ya basi lenye Namba za usajili  T178 DHD lililokuwa likisafiri kutoka Kabwe wilayani Nkasi kuelekea mjini Sumbawanga mkoani Rukwa kuacha njia na kupindukaa huku abiria 25 wakijeruhi na tisa kati yao wakiwa ni majeruhi.
Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Kabwe  Jofrey Kuzumbi alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Mei 5 majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la Malimba katika kata hiyo ya Kabwe.
Alisema gari hilo lilikua limebeba  abiria 43 na waliojeruhiwa ni 25 na kati yao tisa ni mahututi na wamekimbizwa katika hospitali teule ya wilaya Nkasi huku wengine wakipelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa kwa matibabu zaidi kutokana na majeraha waliyoyapata.
Alisema baada ya ajali hiyo kutokea mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Beatrice Nyansio (4) alifariki papo hapo huku mzazi wake akipata majeraha.
Afisa mtendaji huyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi hilo na baada ya ajali hiyo dereva wa gari hilo aliyefahamika kwa jina moja tu la Moses alikimbia na mpaka sasa haijulikani alipo.
Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa George Kyando alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa bado uchunguzi wa ajali hiyo  unaendelea ikiwa ni pamoja na kuendelea kumsaka dereva wa gari hilo ambaye amekimbia ili akamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA