DC TANGAYIKA AKAZA MWENDO DHIDI YA WAHARIFU


Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Mhando amesema,vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo vinaendelea kuwasaka na kuwakamata waharifu mbalimbali wanaohatarisha usalama wa raia na mali zao ili kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Muhando ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kuhusu utekelezaji wa agizo lake alilolitoa hivi karibuni akiwataka wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha ambapo amesema silaha tatu zimekamatwa.
Aidha pamoja na mambo mengine Mhando amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kupambana na uharifu unaojitokeza huku akiwataka wanaomiliki silaha bila kibali halali kuendelea kuzisalimisha ili kuepuka mkono wa sheria.
Wakazi wilayani Tanganyika wanataja miongoni mwa matukio yanayotokea mbali na mauaji kuwa ni uporaji wa mali za raia nyakati za usiku tangu kuanza mwaka 2018.
Januari 22 mwaka huu,mkuu wa Wilaya Salehe Mhando akiwa ziarani kata ya Kasekese alitoa agizo kwa wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalmisha kabla ya msako kuanza baada ya Februari 4 mwaka huu.
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA