WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA HATARINI KUPATA KIPINDUPINDU


Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Luhafwe kata ya Tongwe wilayani Tanganyika Mkoani Katavi wamesema,wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko kuokana na maji wanayotumia kutokuwa safi na salama.
Wakazi hao wameiambia Mpanda Radio kuwa,chanzo cha maji wanachokitegemea ambacho hakina maji safi na salama, kinaingiliwa na taka mbalimbali ambazo ndizo zinazosababisha wao kuumwa matatizo ya tumbo mara kwa mara.
Aidha wamesema wanalazimika kutumia maji hayo kwa sababu hakuna chanzo kingine kinachoweza kuwapatia maji.
Kwa mjibu mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw.Malaika Bujiku na katibu wake Paul Nkingwa Mabenga wamesema mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando alioneshwa chanzo hicho lakini mpaka sasa hakuna hatua iliyochukuliwa na serikali ili kuwanusuru wananchi na hali hiyo.
Mapema mwaka 2016,serikali ya wilaya ya Tanganyika ilipitisha azimio la kujenga mji wa kibiashara katika eneo la Luhafwe lakini mpaka sasa huduma za kijamii kama shule,afya na maji bado ziko duni ambapo licha ya serikali kuahidi kuwapatia maji safi na salama mpaka sasa hakuna utekelezaji.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA