MWANAFUNZI ALIYEPOTEA TANZANIA APATIKANA AKIWA HAJITAMBUI


Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania, Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliye ripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire akiongea na waandishi wa habari kuelezea tukio la kupatikana kwa Mwananchuo Abdul Nondo 
Inadaiwa kuwa alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo alilo jikuta kuwa yuko wapi? ambao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa kituo cha polisi kilichoko karibu.
Mahojiano yake katika kituo cha Polisi Mafinga eneo alikopatikana yamefanyika na baadaye kupiga simu kwa ndugu zake. Baada ya kupata taarifa ya kupatikana mwanawe,baba mzazi Mussa Mitumba ameomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata mwanae ili aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kutekwa kwake.
Alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne katika afisi za shirika hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nchini humo,Tahliso.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) ulisema baada ya kuondoka afisi hizo, Bw Nondo alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani Madale.
Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.
Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limeeleza kuwa limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama Mwenyekiti wa  Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Omari Nondo alikuwa ametekwa au la ili liweze kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Chanzo:bbc

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA