MAJAMBAZI WAUA,WAJERUHI NA KUPORA MALI MGODINI MKOANI KATAVI



Na.Issack Gerald
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kwa rasasi  sehemu mbalimbali za miili yao baada ya kuvamiwa na majambazi  usiku wa kuamkia leo katika mgodi wa dhahabu wa Isulamilomo uliopo Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi.
Pamoja na kuwataja majeruhi,kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Jaffari Gwiyama Kitambwa,amemtaja aliyefariki kuwa ni Kalister Kalyalya(21) mkazi wa kata ya machimboni Wilayani Mpanda aliyepigwa risasi mgongoni na kutokezea tumboni.
Dkt.Kitambwa amewataja waliojerhiwa kuwa ni  Joseph Panya Mahinja(39) mkazi wa mkoani Morogoro amevunjika mfupa wa bega,Mrisho Abdalla(41) makazi wa Kawajense  alipigwa risasi kifuani upande wa juu na kutokezea begani upande wa kulia,Masunga Mwigulu mkazi wa Kasekese wilayani Tanganyika ambaye alipigwa risasi mkono wa kulia na kuvunjika mfupa wa mguu.
Kwa upande Joseph Panya Mahinja(39) mkazi wa mkoani Morogoro na Mrisho Abdalla makazi wa Kawajense Manispaa ya Mpanda ambao walikuwa wakinunu dhabau hiyo,wamesema tukio la kuvamiwa kwao limetokea jana usiku majira ya saa mbili usiku na limewaathiri kiafya.
Katika hatua nyingine Dkt.Kitambwa amesema kuwa majeruhi wote wanatarajiwa kupelekwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi huo Bw.Amosi Kahega pamoja na mambo mengine amesema mgodi huo wenye wafanyakazi zaidi ya 1000 umepatwa na athari kubwa ikiwemo kupoteza nguvu kazi ya taifa na upotevu wa pesa na dhahabu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda akithibitisha tukio hilo amesema jeshi la polisi limeanza uchunguzi wa tukio hilo.
Hilo ni tukio la pili la linalohusisha ujambazi Mkoani Katavi na kusababisha kifo ambapo mbali na tukio la Januari 22 mwaka huu lililohusisha mwanafunzi kuwawa na mtu anayesadikika kuwa ni mwendesha bodaboda pia kuna tukio la Januari 27 mwaka huu katika kata ya Ugalla ambapo Mtu mmoja aliuwawa na wengine zaidi ya watano kujeruhiwa baada ya uvamizi wa watu wanatajwa kuwa ni mambazi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA