BARAZA LA MADIWANI MPANDA LAONYA WATUMISHI WANAOSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI


Na.Issack Gerald
Baraza la Madiwani Halamshauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,limesema litachukua hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafukuza kazi watumishi wa idara ya ardhi watakaosababisha migogoro ya ardhi baina ya wananchi.
Mstahiki Meya wa Manispaa Mpanda Mh.Willium Mbogo
Tamko hilo ambalo limtolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Willium Mbogo kupitia kikao maalumu cha bajeti cha baraza hilo ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo.
Amesema kumeanza kujitokeza migogoro ya ardhi kuhusiana na kiwanja kimoja kuuzwa kwa watu wawili tofauti suala ambalo limetajwa kufanywa na watumishi wa idara ya ardhi wasio waaminifu na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Willium Mbogo amelazimika kuagiza migogoro hiyo isuluhishwe wao kwa wao kabla ya tatizo kuwa na baraza kupewa taarifa.
Aidha amesema hatua za kisheria zitachukuliwa pia kwa watumishi wa idara mbalimbali ambao wamesababisha Manispaa ya Mpanda Kukosa mapato kutokana na uzembe wao katika uwajibikaji.
Katika Kikao hicho cha siku mbili,mambo mbalimbali yamejadiliwa katika rasmu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018,2019 ikiwemo masuala ya elimu,afya,miundombinu ya barabara pamoja na ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.
Habari zaidi ni kupitia P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA