MASHEHE 5 MKOANI KATAVI WAMEJIUZURU


Na.Issack Gerald
Mashehe watano akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Katavi, Shehe Shaaban Bakari wamesema kujizulu kwao ni kutokana na shehe wa Mkoa wa Katavi kukiuka Katiba ya Bakwata.
Katika picha ni Shehe Mashaka Kakulukulu miongoni mwa waliojiuzuru

Wajumbe waliojiuzulu wakiwemo Mashehe Mohamad Shaaban Sigulu na Said Haruna Omary wamemtuhumu Shehe wa Mkoa Ally Hussein kuwa kinara wa kukiuka katiba ya Bakwata.
Wajumbe wengine wa baraza la mashehe Mkoa waliojiuzuru ujumbe ni Shehe Mashaka Nassoro Kakulukulu na Hassan Mbaruku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bakwata Mkoani Katavi Shehe Shaban Bakari ambaye naye juzi amejiuzuru,amesema Shehe wa Mkoa wa Katavi Ally Hussein amekuwa akizuia maendeleo ya dini ya kiislamu kwa kutokubaliana na maamuzi ya vikao halali huku akiunga mkono waharifu na wanaopinga maendeleo ndani ya dini.
Aidha Shehe Bakari amesema sababu nyingine ambayo imewafanya wajiuzuru ni baada ya shehe wa Mkoa kusema hataki kuundwa kwa uongozi mwingine utakaosimamia ukusanyaji mapato kutoka Miradi ya uchinjaji wa ng’ombe ulipo kata ya Mpanda Hotel na maduka yaliyopo Msikiti mkuu wa Ijumaa ambapo kwa sasa amesema mapato yanaishia mifukoni mwa wachache huku baadhi ya viongozi wa dini hiyo wanaomiliki maduka wakiwa hawalipii tozo na wao kufanyia biashara katika maduka hayo.
Hata hivyo Shehe Ally Hussein amekana tuhuma dhidi yake za kukiuka katiba huku akisema ni fitina na wanatarajia kufanya kikao ili kutoa maazimio kutokana na hali iliyotokea.
Miezi michache iliyopita,Mufti mkuu wa Tanzania Abubakari Zuberi aliwaagiza makatibu wote wa dini ya kiislamu hapa nchini kuainisha mali zinazomilikiwa na dili hilo ambapo kwa mjibu wa sakata ambalo limetokea agizo la mufti halijatekelezwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA