LEO NI SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI

Na.Issack Gerald
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imethibitisha kuwa leo kutakuwa na Maadhimisho ya siku ya watu wenye Ulemavu Duniani.
Kauli hiyo imethibitishwa na Idara za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa jamii za Manispaa hiyo na kuwataka wananchi kujitokeza na kushiriki katika maadhimisho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili.
Miongoni mwa maafisa ambao wamethibitisha kuwepo kwa maadhimisho hayo ni pamoja na afisa maendeleo ya jamii Bi.Marietha Mlozi kutoka idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Mpanda.
Katika Mkoa wa Katavi inakadiriwa kuwa kuna watu wenye ulemavu wapatao zaidi ya 2000 ambao wamegawanyika katika makundi ya wasioona,viungo,ualibino,viziwi na wenye mtindio wa ubongo(Masonji).
Sheria namba 9 ya mwaka 2010 iliyopitishwa na bunge la Tanzania mwaka 2010 inaitaka serikali na jamii kuhakikisha makundi ya watu wenye ulemavu yanapatiwa haki sawa na watu wasio na ulemavu katika haki za kibinadamu.
Kitaifa maadhimisho haya yanayoadhimishwa Desemba 3 ya kila mwaka yataadhimishwa Mkoani Simiyu na kauli mbiyu ya mwaka 2017 inasema‘’Badilika tunapoelekea jamii Jumuishi na imara kwa watu wote’’.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA