JELA MIAKA 30 KWA KUUA TEMBO MKOANI KATAVI

MAHAKAMA ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu Jackison  Eijuel (52) mkazi wa kata ya Katumba kutumikia kifungo cha  miaka 30 jela na kulipa faini ya shilingi milioni 99 baada ya kupatikana na  hatia ya kumiliki na meno manne ya tembo pamoja na vipande vinne vya meno hayo.
Hukumu  hiyo  ilitolewa juzi  na  hakimu   mkazi  mfawidhi wa  mahakama hiyo Chiganga  Tengwa baada ya  kuridhika  na  ushahidi uliotolewa   Mahakamani  hapo  ambapo mshitakiwa  hakuwa na shahidi yoyote kwa upande wake.
Akisoma hukumu  hiyo hakimu Twengwa alisema  mahakama imebaini mtuhumiwa alitenda kosa hilo  kinyume  na  kifungu  cha  sheria  namba 235  cha mwenendo  wa  mashitaka.
Alisema  baada ya  kusikiliza  utetezi wa mshitakiwa ,mahakama imethibisha pasipo kuacha shaka yoyote  kuwa  mshitakiwa  amepatikana  na  hatia kwa  kukamatwa akiwa  na  meno ya  tembo ambayo ni sawa tembo watatu  waliouawa wenye  thamani ya zaidi ya  shilingi milioni 90.
Awali   mwendesha  mashitaka  mwanasheria wa  Serikali Fraviani   Shiyo   alidai mahakamani  hapo  kuwa   mshtakiwa  Jackisoni   Elijuel aliyepewa uraia wa Tanzania ambapo awali alikuwa raia wa Burundi alitenda  kosa hilo  Oktoba  25  mwaka huu  majira ya saa mbili na  nusu  usiku  katika   Kijiji  cha Urwila tarafa ya  Nsimbo  wilayani Mpanda.
Shiyo  aliiambia  mahakama hiyo  kuwa  mshitakiwa alikamatwa  na  askari  maalumu wa  kuzuia  ujangili wa  pori la Ugala  baada ya kupata taarifa  za  mshitakiwa kujihusisha  na  biashara haramu ya kuuza meno ya  tembo.
Aidha Shiyo alieleza kuwa baada ya  askari hao  kupata  taarifa  hizo  ndipo  walipoandaa  mtego na  kumkamata  akiwa  na   meno  ya   tembo manne   mazima  na  vipande  vinne vyenye  uzito wa  kiligramu  27  yenye  thamani ya shilingi milioni 99  ambayo ni  sawa  na tembo watatu wazima.
Mshitakiwa  katika  utetezi  wake  aliomba  mahakama imwachie  huru kwa  kile  alichodai  kuwa   meno ya tembo  aliyokamatwa  nayo  hayakuwa yake bali yalikuwa  ni  ya  mtu mmoja   aliyemtaja kwa  jina la Hussen  Samora  kuwa ndiye   aliyekuwa  amemtuma kuyabeba kwa kutumia  pikipiki  yake  mshitakiwa ili ampelekee.
Baada ya  utetezi huo  kabla ya  hakimu  kusoma hukumu wakiri wa  Serikali Shiyo aliiomba mahakama  itoe adhabu kali kwa   mshitakiwa  ili iwe  fundisho kwa watu  wengine  kwani   vitendo vya  ujangili vimezidi  kushamili katika hifadhi ya Katavi.
Baada ya  kuusikiliza  utetezi  wa  mshitakiwa  hakimu huyo wa alimtaka  mshitakiwa  ataje namba  za  pikipiki  ambayo  alidai ni  mali yake  aliyoitumia   kubebea  meno hayo ya  tembo  na  amekuwa  akiiendesha  kwa kipindi  cha miaka  miwili  hata  hivyo mshitakiwa  alishindwa kuzitaja   namba  hizo za pikipiki   aliyodai ni ya  kwake kitendo kilichothibitisha aliidanganya mahakama kuwa alikodiwa ili pikipiki yake itumike kubeba meno hayo ya tembo. 
Akisoma  hukumu  hiyo  hakimu Tengwa  alisema  mshitakiwa amekutwa  na   hatia  kinyume  na  kifungu  cha   sheria   namba  235 ya mwenendo wa  mashitaka  hivyo  mahakama  imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30  jela na kulipa  faini ya shilingi milioni 99.

Habarika zaidi na P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA