DC MATINGA:MALIASILI WATAJENGA SHULE MBADALA WA NSANDA

Na.Issack Gerald-Mpanda

Sehemu ya majengo ya iliyokuwa shule ya Msingi Nsanda
Mkuu wa wilaya ya Mpanda bi Liliani Matinga amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati wizara ya maliasili ikishughulikia kujenga shule ambayo itakuwa mbadala wa iliyokuwepo katika maeneo ya hifadhi walipoondolewa wananchi.
Moja ya majengo ya vyoo vya iliyokuwa shule ya Msingi Nsanda
Kauli hiyo imetolewa jana na Matinga ambapo amesema shule ya Msingi Nsanda ilijengwa kimakosa katika kijiji ambacho kilikuwa hakijasajiliwa hivyo wizara ya maliasili itayachukua majengo hayo na kujenga shule nyingine katika kijiji kilichosajiliwa.
Ameeleza kuwa taratibu zote zimeshafanyika na tayari wizara ya maliasili imeshakubali kujenga na hivyo wanasubiri utekelezaji kuanza.
Matinga amewaasa wananchi kuwa makini na wawekezaji wanao ingia katika maeneo yao ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

                                          Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA