MH.SAMIA SULUHU HASSANI AONYA MATUMIZI YA KAMERA NA TOCHI KUTOKUWA CHANZO CHA UCHUKI KATI YA SERIKALI NA WANANCHI

NA.Issack Gerald-Moshi Kilimanjaro
MAKAMU wa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amewataka askari wa usalama barabarani kutotumia kamera na tochi kuwanyanyasa wananchi hali inayochochea chuki kati ya serikali na wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassani wakati akizindua wiki ya Nenda kwa usalama uzinduzi ambao umefanyika Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Aidha Makamu wa rais Mh.Samia Suluhu hasani ameliagiza baraza la usalama barabarani kuhakikisha kila anayeendesha chombo cha moto awe na leseni halali huku wamiliki wa mabasi kwa upande wao wakitakiwa kuwa sehemu ya kuzua ajali hapa nchini.
Kwa upande wake baraza la usalama barabarani hapa nchini limesema maadhimisho ya wiki ya nenda klwa usalama barabarani ni sehemu ya mkakati endelevu unaowaelimisha na kuwakumbusha madereva na watumia barabara wote nchini kutambua wajibu wao wawapo barabarani.
Aidha Baraza limesema mpango wa kupambana na ajali hapa nchini kumesaidia kupunguza ajali kwa asilimia 49 katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu.
Kauli mbiyu katika wiki ya nenda kwa usalama mwaka huu ni ‘’Zuia Ajali,Tii sheria Okoa Maisha’’.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA