MADIWANI WANAOTUHUMIWA KUNUNULIWA NA CCM WAHOJIWA NA TAKUKURU



Maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam, wamewahoji kwa zaidi ya saa sita,madiwani waliojiuzulu Chadema wanaotuhumiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Joshua Nassari kuwa walipewa rushwa.

Waliofika Takukuru ni Catherine Mtui,aliyekuwa diwani wa viti maalumu,Japhet Jackson(aliyekuwa diwani wa Ambuleni) na Bryson Isangya (aliyekuwa diwani wa Maroroni).
Baada ya kuhojiwa hawakutaka kuzungumza chochote wakisema wanaacha uchunguzi uendelee.
Pamoja nao, diwani wa Mbuguni,Ahimidiwe Rico anayedaiwa kuwa ndiye alirekodi sauti na picha wakati akishawishiwa na viongozi wa Serikali na wa Halmashauri ya Meru amehojiwa kwa zaidi ya saa tatu jana Jumanne Oktoba 17, 2017.
Rico amesema amewaeleza Takukuru kila kitu ambacho anakifahamu katika sakata hilo, ikiwemo kuwarekodi viongozi ambao walimshawishi kujiuzuru udiwani.

Rico aliyesindikizwa na diwani wa  Nkwanankore, Wilson Nanyaro amesema  ana imani na Takukuru kwamba watafanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua.

Alisema baada ya mahojiano yaliyoanza saa tatu hadi saa sita mchana, maofisa wa Takukuru walimwambia aondoke na watamuita watakapomuhitaji.

Hakuna ofisa wa Takukuru aliyekuwa tayari kuzungumzia mahojiano hao wakisema wasemaji ni makao makuu ya ofisi hiyo Dar yaliyoko jijini Dar es Salaam.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA