HALMASHAURI YA WILAYA NSIMBO MKOANI KATAVI WANAFUNZI 14 WAPATA UJAUZITO



Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
Moja ya picha ya wanafunzi Mkoani Katavi
JUMLA ya wanafunzi 14 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wamepata ujauzito katika kipindi cha mwezi Januari hadi juni mwaka huu.

Afisa ustawi wa jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi.Dianarose Mnuo amesema miongoni mwa mambo yanayochangia wanafunzi kupata mimba wakiwa mashuleni ni kutokuwa na mabweni,wazazi kutowalinda watoto,umbali anakotoka mwanafunzi pamoja na umaskini.
Amesema kati ya wanafunzi hao 14,wanafunzi watano wanatoka shule ya msingi Ugalla,Katumba na Kanoge huku 9 waliopo katika Shule za sekondari wakitoka shule za sekondari Katumba yenye wanafunzi 3,Sule ya Sekondari Nsimbo wanafunzi 5 na sitalike 1.
Hata hivyo amesema kumekuwa na changamoto ya wasichana wanaopewa ujauzito kuwataja wahusika wanaowapa mimba pamoja na wahusika wa pande mbili kupeana rushwa ili kumaliza tatizo wao wenyewe kwa wenyewe.
Katika kukabiliana na baadhi ya changamoto,Halmashauri imekusudia kujenga mabweni ya wasichana ikiwemo katika shule ya Sekonadri Nsimbo ambapo wapo katika mchakato.
Kwa mjibu wa Afisa Ustawi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Kesi zote 14 zimeripotiwa katika vyombo vya sheria ambapo hata hivyo hakuna ripoti inayoonesha kutolewa adhabu kali kwa wanaowapa mimba wanafunzi Mkoani Katavi.
Kutokana na Mkoa wa Katavi kuongoza kwa asilimia 45 katika mimba za utotoni,mkoa wa Katavi unatarajia kufanya maadhimisho hayo kimkoa katika Manispaa ya Mpandahuku ikitanguliwa na kongamano litakalofanyika leo ili kujadili matatizo ya mtoto wa kike  ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku kike Duniani kitaifa yakiadhimishwa Mkoani Mara.
Katika maadhimisho hayo yanayoadhimishwa Oktoba 11 ya kila mwaka,Kaulimbiyu kwa mwaka huu inasema’’Siku ya kimataifa ya mtoto wa kike,tokomeza mimba za utotoni tufikie uchumi wa viwanda’’
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA