WAKAZI KATAVI WALALAMIKIA MATUSI YA WAGUZI NA KUNYIMWA MATIBABU-Septemba 12,2017

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Katumba Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi,wamewalalamikia baadhi ya wauguzi na madaktari wa kituo cha afya cha Katumba na Zahanati ya Kaminula kutokana na  lugha ya matusi kwa wagonjwa inayoambatana na kutopatiwa matibabu ipasavyo.

Wakazi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao wakihofia usalama na kunyimwa matibabu katika vituo hivyo wamesema tatizo la baadhi ya wagonjwa kunyanyaswa lipo kwa muda mrefu ambapo limekuwa halichukuliwi hatua ya utatuzi licha ya Diwani,Afisa Mtedaji wa Kata,Mbunge na Halmshauri kuwa na taarifa ya hali ilivyo.
Aidha baadhi ya wakazi wa Katumba wamelalamika kufukuzwa na kunyimbwa matibabu wanapohoji tatizo la kutokuwepo kwa umeme katika katika kituo cah afya Katumba licha ya Shirika la wakimbizi duniani UNHCR na Kanisa la FPCT kuleta sola na betri katika kituo hicho ambapo kwa sasa wagonjwa hao wanalazimika kwenda wakiwa na tochi au taa kwa ajili ya mwanga.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa kituo cha afya cha Katumba Dkt.Gabriel Ngonyani amekataa kuzungumza na Mpanda Mpanda Radio kuhusiana na malalamiko hayo kwa madai kuwa mpaka apate kibali cha mwajiri wake.
Wakati huo baadhi ya wagonjwa wanaotegemea kupata huduma ya afya katika zahanati ya Kaminula akiwemo mkazi mmoja ambaye amejitambulisha kwa majina ya Vastina Evarist  wamedai wanalazimika kutopatiwa huduma na waguguzi katika zahanati ya Kaminula mpaka wanapokuwa wamekubali kuchota maji kwa ajili ya wauguzi na asipokubali kuchota maji inabidi arudi nyumbani bila kupata matibabu.
Diwani wa Kata ya Katumba Mh.Seneta Baraka amekili kupokea kwa tuhuma hizo kwa wauguzi katika kituo cha afya cha Katumba pamoja na zahanati ya Kaminula.
Aidha Mh.Seneta Baraka pamoja mambo mengine amesema tatizo la umeme kituo cha afya katumba licha ya kuwa sola na betri zilinununuliwa kama wananchi wanavyodai isipokuwa anachofahamu ni kuwa betri zilisharibika isipokuwa hana taarifa za uhakika kuwa betri hizo zinatumiwa na watumishi wa afya wa kituo hicho katika majumba yao ambapo amesema tayari Shilingi milioni 1 imetengwa ili kununua betri kuondoa tatizo la ukosefu wa umeme kwa takibani mwaka mzima.
Kwa mjibu wa wakazi wa Kata ya Katumba Jumla ya Sola 11 na Betri tatu zililetwa na UNHCR pamoja na Kanisa la FPCT.
Katika hatua nyingine kata ya Katumba yenye vijiji 16 ikiwa na wakazi zaidi ya 54,700 wanaotegemea kupata huduma za afya katika kituo cha afya Katumba wakazi hao wameongeza kuwa licha ya Diwani,Afisa Mtedaji wa Kata,Mbunge na Halmshauri hadi ngazi ya kuwa na taarifa ya hali ilivyo katika huduma za afya pia wamesema hali imekuwa mbaya zaidi hasa katika huduma ya maji na miundombinu ya barabara.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com  
0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA