TANESCO MKOANI KATAVI WAMEWASHA UMEME WA REA WILAYANI MLELE-Septemba 13,2017

SHIRIKA la umeme Nchini Tanesco Mkoani Katavi limewasha umeme wa mradi wa umeme vijijini Rea Wilayani Mlele Mkoani Katavi na kuwataka wananchi Wilayani humo hususani wakazi wa mji wa Inyonga ambayo ni makao Makuu ya Wilaya watandaze nyaya zao katika nyumba ili waunganishiwe umeme.

Meneja wa Shirika hilo Mkoani Katavi Mhandisi Julius Sabu akizungumza na wakazi wa Inyonga katika viwanja vya shule ya msingi Inyonga pamoja na mambo mengine umeme huo wa REA ambao ni wa awamu ya pili unawanuafaisha wakazi wa vijiji sita ambavyo ni Kijiji cha Utende, Wachawaseme, Mtakujua, Kanoge,Inyonga namba 1 na Inyonga namba 2.
Aidha Mhadisi Sabu amesema kila kijiji kina kimefungiwa transfoma yake ambapo amewataka wakazi wa vijiji hivyo kulinda transfoma hizo ili zisiharibiwe na kwa kuwa baadhi zimefungwa katika sehemu ambapo hakuna makazi ya watu kutokana na ramani inayoonesha nguzo zinakotakiwa kupita.
Kwa upande wake Afisa mahusiano wa wateja waTanesco Mkoani Katavi Bw.Amon Michael amesema elimu imetolewa kuhusu matumizi ya umeme ikiwemo kutofautisha wajibu wa mkandarasi mdogo na Mkandarasi Mkubwa Mkandarasi pamoja na aina ya nyumba zinazotakiwa kuunganishiwa umeme huku akisema nyumba inayotakiwa kuunganishiwa umeme inatakiwa iwe ya bati na iwe ndani ya mita 30.
Naye Meneja wa Tanesco Wilayani Mlele Mhandisi Bw.Chacha Nsiku amewashauri wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme wachukue fomu mapema na kutandaza nyaya haraka ili wananchi wanaufaike na umeme.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi Wilayani Mlele pamoja na kuwapongeza Tanesco kwa kuwasha umeme,wamesema umeme huo utawasaidia kufanya shughuli zao kwa uhakika na kukuza uchumi wao.
Hata hivyo wamehofia kuwa huenda tatizo la kukatika kwa umeme likawa kubwa kama ilivyokuwa awali kabl aya umeme huo ambao Shirika la Tanesco limwahakikishia kuwa umeme huo ni wa Uhakika.
Kwa mjibu wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco kuhusiana na mradi wa umeme wa vijijini,mwananchi anachangia shilingi 27,000/= ili aunganishiwe umeme.
Mwezi Juni Mwaka huu,wakazi Wilayani Inyonga walikuwa wakilalamika kukosa nishati ya umeme na kushindwa kufanya shghuli zao za maendeleo.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com
0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA