SUMATRA,KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI RUKWA WATAKIWA KUTOA ELIMU ILI KUDHIBITI AJALI-Septemba 9,2017

JESHI la polisi Mkoani Rukwa limeitaka mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumtra pamoja na kikosi cha  usalama barabarani kujitahidi kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani humo ACP George Kyando wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.
Kamanda Kyando amesema Sumtra pamoja na kikosi cha  usalama barabarani kujitahidi kutoa elimu hasa watumia vyombo vya moto kuwa makini wanapokuwa barabarani kwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani huku wakiwajali watembea kwa miguu.
Kauli ya jeshi hilo inakuja baada ya juzi watu wawili kufariki kwa ajali na wengine sita kujeruhiwa katika matukio mawili tofauti ambapo chanzo kikuu kimebainika kuwa ni mwendokasi wa madereva wa vyombo vya ufasiri.
Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa ACP George Kyando juzi Septemba 7 katika kijiji cha Kamawe kata ya Sundu ambapo kulitokea ajali ambayo ilihusisha gari aina ya Noah yenye namba za usajili T 549 DFK Noah mali ya kanisa la Moravian Mwimbi ikiendeshwa na dereva mwenye umri wa miaka 40 na ilisababisha vifo vya watu wawili ambao ni Winfrida Simoni(35) na mtoto Shama Charula(mwaka mmoja) wote wakazi wa kijiji cha Mwimbi.
Aidha kamanda Kyando amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Joyce Namzyemba(27),Dalila Kalito,Rucia Pesa(30),Jeneroza Nkasu na Balubina Ndasi wote wakazi wa kijiji cha Mwimbi.
Aidha ajali nyingine iliyotokea juzi kijiji cha Tamasenga Manispaa ya Sumbawanga ikihusisha gari yenye namba za usajili STK 360 Mali ya Halimashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ikiendeshwa na dereva mwenye umri wa 48 ilimgonga mtembea kwa miguu mtoto wa miaka saba na kumsababishia majeruhi mwilini.
Kamanda Kyando alisema Chanzo cha ajali ni uzembe  wa dereva kutokujali watumiaji wengine wa barabara.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA